Jumatatu, 2 Machi 2015

Dunia inaendeshwa NaKanuni za kibiashara.

Somo; Dunia inaendeshwa Na
             Kanuni za kibiashara.
Mchungaji; Goodlucky Kyara
HUDUMA YA NEW VINE CHURCH
luka 19:14-27, mathayo 25:14-27
Kila mtu ni mfanya biashara
Mfano: wasomi wanauza ujuzi wao, makuli wanauza nguvu zao Na wamiliki wa makampuni wanauza bidhaa Na huduma mbali mbali.

KANUNI ZA BIASHARA
1. Mungu ndio mmiliki wa mali zote . zaburi 24: 2
2. Mungu amempa kila mtu kitu chake. Kila mtu ana mtaji na mtaji sio pesa pekee. Mtaji wako ndio mbegu au kianzio chako wajibu wako ni wewe kuzalisha tunda au matokeo.

AINA ZA MITAJI ULIYONAYO
1. Pumzi au uhai wako.
Bila kuwa na uhai na afya huwezi kufanya biashara yoyote. 'Usitumie maisha yako wekeza maisha yako'. 'Don't spend your life , invest your life'
2. Muda.
Matumizi ya muda ndio yanayoamua mafanikio yako. Watu wengi wanaweza kuajiriwa kwa sababu kujiajiri kuna hitaji nidhamu ya hali ya juu kuhusu matumizi ya muda. Matajiri huwa muda wao hauwatoshi ndio maana huwa wananunua muda wa watu wengine kwa kuwaajiriwa ili kuzidisha uzalishaji wa kampuni zao.
3. Akili au ufahamu
Kila mtu anayezaliwa mwenye akili timamu anaweza kufanya biashara yoyote. Ukosefu wa mawazo Na fikra au akili za kubuni biashara yoyote ni kitu kibaya sana.
4. Elimu
Kila maarifa au ujuzi ulionao ni mtaji tosha.
5. Nguvu
Nguvu ulizonazo pia ni mtaji.
6. Sauti.
Kama una sauti nzuri unaweza kufanya biashara yoyote inayohusiana na sauti. Mfano kuwa mshehereshaji na mtengenezaji wa matangazo ya ki biashara. Steve wonder ambaye ni mwanamuziki maarufu duniani ambaye ana ulemavu wa macho amewahi kusema hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa na macho ambayo hayaoni . Hapa inamaanisha kutokuona fursa na mitaji mbali mbali uliyonayo
7. Kipaji
Mfano kucheza mpira , kuchora n.k.

AINA ZA MALI
1.Mali zinazokula mali.
Mfano gari ya kutembelea ambayo haikuongezei uzalishaji wako zaidi ya kukuongezea matumizi yako. Hapa tuna weza kuongelea gari za mikopo alafu haikuingizii kipato.
2. Mali isiyokula mali ila pia haizalishi Mali yoyote
Samani za majumbani kwetu mfano sofa za makochi na meza.
3. Mali inayozalisha mali.
Mfano daladala au hata pia gari binafsi isiyo kuingiza kwenye madeni na pia inaongeza uzalishaji wako kibiashara.

Mafanikio yanakuja kwa kuwa Na mali zinazozalisha KULIKO mali ambazo hazizalishi Na pia hazili mali zingine KULIKO mali zinazokula mali zingine.

Kumbuka kiwango cha kuheshimiwa kwako kinategemea
Kiwango cha uzalishaji wako katika kufanya biashara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni