Jumatatu, 2 Machi 2015

SEMINA YA MALENGO YA MAISHA








SEMINA YA MALENGO YA MAISHA


SOMO: MALENGO YA FAMILIA
MHUBIRI: MTUMISHI BUSARA
KANISA LA T.A.G – NYAMALANGO, MWANZA. TANZANIA.
Mathayo 19:10 inasema kwamba kama ya mke na mume yako hivi haifai kuoa. Kabla hujaingia kwenye ndoa lazima uanze kiroho yaani ufuate taratibu zote za kiimani ya kikristo kama mtu aliyeokoka. Kabla ujaingia kwenye tafuta kuwa na ufahamu juu ya masuala ya ndoa la sivyo utaichukia ndoa.
Somo hili limegawanyika katika vipengele vine navyo ni:-
A) Utangulizi
B) Wajibu wa mume
C) Wajibu wa mke
D) Wajibu wa mtoto

UTANGULIZI
1.Mungu aliumba mtu mume na mtu mke kwa maana hio alikusudia waanzishe familia. Mwanzo 1:26-27 inaonyeshwa Mungu baada ya uumbaji aliweka kanuni ya maongezeko kwa mwanadamu. Hapa Mungu aliruhusu kanuni ya maongezeko ( principle of multiplication) katika kila Nyanja ya Maisha mfano uzazi, biashara, kazi n.k. Ukiamua kuwa mzalishaji utapata faida. Yesu alisema tawi lisilozaa lafaa kukatwa likatupwe motoni. Kutengeneza faida ni halali kwa kila mkristo na sio dhambi wala vibaya. Ukishindwa kuzalisha Mungu amakuona wewe ni mbaya tena ni mlegevu.
2. Wote tunafanana kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu japo tunatofautiana kimaumbile tu.
3. Mamlaka ya kutawala ni kwa mwanaume na mwanamke. Mwanzo sura ya kwanza inasema kisha mkatawale viumbe vyote vya baharini, ardhini na nchi kavu.
KUMBUKA: Baada ya mwanadamu kufanya dhambi Mungu alimuadhibu mwanadamu ila punde tu pale tunapookoka tunarudi bustani ya edeni na tunabadili majina na Kuitwa wabarikiwa na sio walaaniwa tena.
4. Nguvu ya uzalishaji iliwekwa ndani yetu kila mmoja. Mungu alisema nendeni mkaitunze na kuilima bustani kisha mpate mzao na matunda. Waume tuwaruhusu wake zetu kufanya kazi na biashara kwa sababu wote tumepewa nguvu ya uzalishaji.
3. Wote wawili walikaa wazi. Wote walikuwa uchi. Lazima kwenye ndoa pawe na uwazi kwenye mapato na matumizi ya pesa. Usiri huaribu ndoa bali uwazi.

WAJIBU WA WAUME AU MWANAUME NDANI YA FAMILIA NA NDOA YAKE.
1Petro 3:7 inawaasa waume kukaa na wake zao kwa akili, wakiwaheshimu ili maombi yao yasizuiliwe. Waefeso 5:25-29 inasema kwa ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
1. Wajibu wa kwanza wa mwanaume au mume ni kuwa kiongozi wa familia. Kutoka kwa mstari wa biblia hapo juu, biblia inasisitiza waume kutumia akili zao ipasavyo kujibu maswali ya kwa nini, wapi, kivipi na yupi yanayojibijika baada ya kufikiri. Wake wanapenda kuulizwa maswali hayo hivyo waume yawapasa kufikiri kwa makini.
2. Kumheshimu mke wake. Biblia iansema kwamba umpe heshima mke wako. Afrika tuna changamoto ya mfumo dume. Mke ni mtu adhimu Mungu aliyokupa wewe mume hivyo yakupasa kumheshimu na kumthamini mkeo hata kama ana mapungufu fulani. Tanzania tuna changamoto ya mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke au mke. Wewe mwanaume jijengee tabia ya kumheshimu mwanamke yoyote.
3. Msifie mkeo. Zungumza juu ya sifa na uzuri wa mkeo. Muite mrembo na hata jamii yako ifahamu.
4. Haki ya urithi. Mithali 13:22 Baba mwema uwaachia urithi wana wake na hata wana wa wanawe ( wajukuu zake ). Mwanaume au ume una wajibu wa kutafuta na kukusanya fedha na mali za kutosha kwa ajili ya mke, watoto na wajukuu zake.
5. Mpende mke wako. Upendo ni kumjali mkeo na kumsikiliza. Mfano kumpa zawadi. Kuna msemo unasema kwamba kiongozi mzuri ni yule aliye msikilizaji mzuri. Pia msemo mwingine unasema unaweza ukatoa kitu bila kumpenda mtu bali hauwezi kumpenda mtu bila kumpa kitu.
6. Unyenyekevu. Efeso 5:21 inasema kwamba inabidi kunyenyekeana katika kimo cha kristo. Je kuna utofauti kati ya upole na unyenyekevu? Upole sio unyenyekevu. Mungu huwapiga na hawapendi watu wenye kiburi. Unyenyekevu ni hali ya kumtanguliza mtu mwingine kuliko wewe. Unyenyekevu unajifunza hauzaliwi nao. Unyenyekevu ni wa muhimu hasa ndani ya ndoa hii inahusisha mme na mke pia. Ukitaka kuongoza watu lazima uwe mnyenyekevu.
7. Kutoa mahitaji ya familia mfano chakula, maladhi na nguo. 1Timotheo 5:8 hii inaelezea kwamba ukishindwa kuleta mahitaji ya familia kama mwanaume au mume wewe ni mbaya kuliko asiyeamini(mfano mchawi au mlevu). Kabla ya kuoa lazima uangalie kama una uwezo wa kutunza familia.

WAJIBU WA MKE AU MWANAMKE NDANI YA FAMILIA AU NDOA YAKE.
Waefeso 5: 22-33 Mtii mumeo kama unavyomtii bwana kwa maana mume ni kichwa cha familia kama bwana alivyo kichwa cha kanisa. Utii huu ni kwa kila jambo na ni utii wa hali ya juu sana.
1. Wajibu wa kwanza wa mke ni kumtii mume wake. Mfano Sara mke wa Ibrahimu alimtii mume wake kama alivyomtii bwana. Mfano Ibrahimu alimwita mke wake dada katika nchi ya ugenini ila Sara alitii.
2. Heshimu uongozi wa mume wako kwa sababu yeye ndio kichwa na wewe kama mke ni msaidizi. Kumheshimu mume wako ni kutambua uwepo wake.
3. Kupanga mambo ya ndani ya nyumba mfano usafi, upishi na kupanga wajibu wa wajakazi wake na pia kuamka mapema asubuhi. Mithali 31:15
4. Kuaminika na kutegemewa. Mithali 31:11 kuaminika katika kila jambo na uaminifu lazima uthibitishwe haiji hivi hivi. Mfano matumizi ya hela.
5. Kutenda wema. Mithali 31:12. Usirudishe baya kwa baya bali baya kwa wema. Usipange kulipiza kisasi. Mithali 17:13 mabaya hayataondoka nyumbani mwako. Kumbuka ugomvi wa ndoa unaathiri mpaka watoto.
6. Kusema maneno mazuri. Mithali 31: 26 sheria ya wema ipo katika ulimi. Zungumza mambo mazuri ya nyumbani mwako mjibu vizuri mme wako. Jifunze kumwambia mme wako sifa zake angalau hata kwa sekunde 15 huku ukimsalimia kwa kumshika mkono ukimuangalia machoni kwa tabasamu ang’avu.
7. Mlinde mume wako Yeremia 31:22 mwanamke ana mlango wa sita wa fahamu kwa sababu huwa wana uwezo wa kuhisi hatari hata kabla haijatokea, waume nao wanatakiwa kuwasikiliza wake juu ya maonyo mbali mbali wanayopewa kwenye maisha.

WAJIBU WA MTOTO
Mtoto ni mtu yoyote aliyezaliwa na wazazi haimaanishi tu wale wenye umri mdogo tu kwa hiyo kila mtu ni mtoto kwa sababu amezaliwa na wazazi. Waefeso 6:1-3 Enyi watoto waheshimuni wazazi.
1. Wajibu wa kwanza ni kuwaheshimu wazazi wako wa kiroho. Hapa tunaangalia wachungaji wetu hata kama umemzidi elimu au fedha. Chunga kauli zako juu ya watumishi wa Mungu. Jifunze jinsi ya kuchukuliana na mapungufu au makosa ya viongozi wako wa kiroho.
2. Tii wazazi wako wa kimwili yaani baba na mama yako. Usiwazungumzie wazazi wako vibaya. Onyesha upendo wako sio tu kwa maneno bali kwa vitendo pia.
3. Usimalaani baba na mama yako. Mithali 20:20 Taa yako inayowaka itazimika ghafla. Hii inamaanisha mambo yako yataharibika mfano kazini, masomoni na nyumbani. Mithali 23:22 Msikilize baba yakow ala usimdharau mama yako akiwa mzee.
4. Usiwaibie wazazi wako. Mithali 28:24 Aibaye mali za wazazi wake huyo ni rafiki wa mtu mharibirifu.
5. Usipoteze mali za wazazi wako. Mithali 19:26 Apotezaye mali za babaye na kumfukuza mama yake ni mwana aniaibishaye na kuleta lawama. Tusifukuze wazazi wetu pale tunapooa au wasichana kuolewa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni