SEMINA
YA MALENGO YA MAISHA
SOMO: MALENGO YA FAMILIA
MHUBIRI:
MTUMISHI BUSARA
KANISA
LA T.A.G – NYAMALANGO, MWANZA. TANZANIA.
Mathayo
19:10 inasema kwamba kama ya mke na mume yako hivi haifai kuoa. Kabla hujaingia
kwenye ndoa lazima uanze kiroho yaani ufuate taratibu zote za kiimani ya
kikristo kama mtu aliyeokoka. Kabla ujaingia kwenye tafuta kuwa na ufahamu juu
ya masuala ya ndoa la sivyo utaichukia ndoa.
Somo
hili limegawanyika katika vipengele vine navyo ni:-
A)
Utangulizi
B)
Wajibu wa mume
C)
Wajibu wa mke
D)
Wajibu wa mtoto
UTANGULIZI
1.Mungu
aliumba mtu mume na mtu mke kwa maana hio alikusudia waanzishe familia. Mwanzo
1:26-27 inaonyeshwa Mungu baada ya uumbaji aliweka kanuni ya maongezeko kwa
mwanadamu. Hapa Mungu aliruhusu kanuni ya maongezeko ( principle of
multiplication) katika kila Nyanja ya Maisha mfano uzazi, biashara, kazi n.k.
Ukiamua kuwa mzalishaji utapata faida. Yesu alisema tawi lisilozaa lafaa
kukatwa likatupwe motoni. Kutengeneza faida ni halali kwa kila mkristo na sio dhambi
wala vibaya. Ukishindwa kuzalisha Mungu amakuona wewe ni mbaya tena ni mlegevu.
2.
Wote tunafanana kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu japo tunatofautiana
kimaumbile tu.
3.
Mamlaka ya kutawala ni kwa mwanaume na mwanamke. Mwanzo sura ya kwanza inasema
kisha mkatawale viumbe vyote vya baharini, ardhini na nchi kavu.
KUMBUKA:
Baada ya mwanadamu kufanya dhambi Mungu alimuadhibu mwanadamu ila punde tu pale
tunapookoka tunarudi bustani ya edeni na tunabadili majina na Kuitwa wabarikiwa na sio
walaaniwa tena.
4.
Nguvu ya uzalishaji iliwekwa ndani yetu kila mmoja. Mungu alisema nendeni
mkaitunze na kuilima bustani kisha mpate mzao na matunda. Waume tuwaruhusu wake
zetu kufanya kazi na biashara kwa sababu wote tumepewa nguvu ya uzalishaji.
3.
Wote wawili walikaa wazi. Wote walikuwa uchi. Lazima kwenye ndoa pawe na uwazi
kwenye mapato na matumizi ya pesa. Usiri huaribu ndoa bali uwazi.
WAJIBU WA WAUME AU MWANAUME NDANI YA FAMILIA NA NDOA YAKE.
1Petro
3:7 inawaasa waume kukaa na wake zao kwa akili, wakiwaheshimu ili maombi yao
yasizuiliwe. Waefeso 5:25-29 inasema kwa ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
1.
Wajibu wa kwanza wa mwanaume au mume ni kuwa kiongozi wa familia. Kutoka kwa
mstari wa biblia hapo juu, biblia inasisitiza waume kutumia akili zao ipasavyo
kujibu maswali ya kwa nini, wapi, kivipi na yupi yanayojibijika baada ya
kufikiri. Wake wanapenda kuulizwa maswali hayo hivyo waume yawapasa kufikiri
kwa makini.
2.
Kumheshimu mke wake. Biblia iansema kwamba umpe heshima mke wako. Afrika tuna
changamoto ya mfumo dume. Mke ni mtu adhimu Mungu aliyokupa wewe mume hivyo
yakupasa kumheshimu na kumthamini mkeo hata kama ana mapungufu fulani. Tanzania
tuna changamoto ya mila na desturi zinazomkandamiza mwanamke au mke. Wewe
mwanaume jijengee tabia ya kumheshimu mwanamke yoyote.
3.
Msifie mkeo. Zungumza juu ya sifa na uzuri wa mkeo. Muite mrembo na hata jamii
yako ifahamu.
4.
Haki ya urithi. Mithali 13:22 Baba mwema uwaachia urithi wana wake na hata wana
wa wanawe ( wajukuu zake ). Mwanaume au ume una wajibu wa kutafuta na kukusanya
fedha na mali za kutosha kwa ajili ya mke, watoto na wajukuu zake.
5.
Mpende mke wako. Upendo ni kumjali mkeo na kumsikiliza. Mfano kumpa zawadi.
Kuna msemo unasema kwamba kiongozi mzuri ni yule aliye msikilizaji mzuri. Pia
msemo mwingine unasema unaweza ukatoa kitu bila kumpenda mtu bali hauwezi
kumpenda mtu bila kumpa kitu.
6.
Unyenyekevu. Efeso 5:21 inasema kwamba inabidi kunyenyekeana katika kimo cha
kristo. Je kuna utofauti kati ya upole na unyenyekevu? Upole sio unyenyekevu. Mungu
huwapiga na hawapendi watu wenye kiburi. Unyenyekevu ni hali ya kumtanguliza
mtu mwingine kuliko wewe. Unyenyekevu unajifunza hauzaliwi nao. Unyenyekevu ni
wa muhimu hasa ndani ya ndoa hii inahusisha mme na mke pia. Ukitaka kuongoza
watu lazima uwe mnyenyekevu.
7.
Kutoa mahitaji ya familia mfano chakula, maladhi na nguo. 1Timotheo 5:8 hii
inaelezea kwamba ukishindwa kuleta mahitaji ya familia kama mwanaume au mume
wewe ni mbaya kuliko asiyeamini(mfano mchawi au mlevu). Kabla ya kuoa lazima
uangalie kama una uwezo wa kutunza familia.
WAJIBU
WA MKE AU MWANAMKE NDANI YA FAMILIA AU NDOA YAKE.
Waefeso
5: 22-33 Mtii mumeo kama unavyomtii bwana kwa maana mume ni kichwa cha familia
kama bwana alivyo kichwa cha kanisa. Utii huu ni kwa kila jambo na ni utii wa
hali ya juu sana.
1.
Wajibu wa kwanza wa mke ni kumtii mume wake. Mfano Sara mke wa Ibrahimu alimtii
mume wake kama alivyomtii bwana. Mfano Ibrahimu alimwita mke wake dada katika
nchi ya ugenini ila Sara alitii.
2.
Heshimu uongozi wa mume wako kwa sababu yeye ndio kichwa na wewe kama mke ni
msaidizi. Kumheshimu mume wako ni kutambua uwepo wake.
3.
Kupanga mambo ya ndani ya nyumba mfano usafi, upishi na kupanga wajibu wa
wajakazi wake na pia kuamka mapema asubuhi. Mithali 31:15
4.
Kuaminika na kutegemewa. Mithali 31:11 kuaminika katika kila jambo na uaminifu
lazima uthibitishwe haiji hivi hivi. Mfano matumizi ya hela.
5.
Kutenda wema. Mithali 31:12. Usirudishe baya kwa baya bali baya kwa wema.
Usipange kulipiza kisasi. Mithali 17:13 mabaya hayataondoka nyumbani mwako.
Kumbuka ugomvi wa ndoa unaathiri mpaka watoto.
6.
Kusema maneno mazuri. Mithali 31: 26 sheria ya wema ipo katika ulimi. Zungumza
mambo mazuri ya nyumbani mwako mjibu vizuri mme wako. Jifunze kumwambia mme
wako sifa zake angalau hata kwa sekunde 15 huku ukimsalimia kwa kumshika mkono
ukimuangalia machoni kwa tabasamu ang’avu.
7.
Mlinde mume wako Yeremia 31:22 mwanamke ana mlango wa sita wa fahamu kwa sababu
huwa wana uwezo wa kuhisi hatari hata kabla haijatokea, waume nao wanatakiwa
kuwasikiliza wake juu ya maonyo mbali mbali wanayopewa kwenye maisha.
WAJIBU
WA MTOTO
Mtoto
ni mtu yoyote aliyezaliwa na wazazi haimaanishi tu wale wenye umri mdogo tu kwa
hiyo kila mtu ni mtoto kwa sababu amezaliwa na wazazi. Waefeso 6:1-3 Enyi
watoto waheshimuni wazazi.
1.
Wajibu wa kwanza ni kuwaheshimu wazazi wako wa kiroho. Hapa tunaangalia
wachungaji wetu hata kama umemzidi elimu au fedha. Chunga kauli zako juu ya
watumishi wa Mungu. Jifunze jinsi ya kuchukuliana na mapungufu au makosa ya
viongozi wako wa kiroho.
2.
Tii wazazi wako wa kimwili yaani baba na mama yako. Usiwazungumzie wazazi wako
vibaya. Onyesha upendo wako sio tu kwa maneno bali kwa vitendo pia.
3.
Usimalaani baba na mama yako. Mithali 20:20 Taa yako inayowaka itazimika
ghafla. Hii inamaanisha mambo yako yataharibika mfano kazini, masomoni na
nyumbani. Mithali 23:22 Msikilize baba yakow ala usimdharau mama yako akiwa
mzee.
4.
Usiwaibie wazazi wako. Mithali 28:24 Aibaye mali za wazazi wake huyo ni rafiki
wa mtu mharibirifu.
5.
Usipoteze mali za wazazi wako. Mithali 19:26 Apotezaye mali za babaye na
kumfukuza mama yake ni mwana aniaibishaye na kuleta lawama. Tusifukuze wazazi
wetu pale tunapooa au wasichana kuolewa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni